
Mkuu wa wilaya ya Muleba, Toba Nguvila.
Agizo hilo limetokana na kufika katika chanzo cha maji cha Kaigara na kukuta baadhi ya wananchi wakifua nguo katika chanzo hicho, na kwamba mbali na kufua na kuoga taka wanazotupa katika vyanzo hivyo zinaweza kuwa na kemikali zinazoweza kuleta madhara kwa binadamu.
"Ni vizuri wananchi kama unataka kufanya shughuli za usafi mfano kufua, chota maji yako peleka pembeni mbali kidogo na chanzo cha maji, lengo ni kuwatunza wenzako na kujitunza mwenyewe, ili haya maji ambayo wanakwenda kutumia wenzako wasiathiriwe kwenye miili yao, wabaki kuwa salama na maji iwe ni kwa ajili ya uhai isigeuke kuwa ni adhabu na madhara katika miili ya binadamu" amesema Nguvila.