Monday , 20th Jun , 2022

Mbunge wa Mvumi Livingstone Lusinde, amesema kwamba jambo alilolifanya Rais Samia la kuwahamisha wamaasai pamoja na Ng'ombe zao kwa mabasi na malori ni jambo la kiungwana na ameonesha ubinadamu na utu.

Mbunge wa Mvumi Livingstone Lusinde

Lusinde ametoa kauli hiyo hii leo Juni 20, 2022, Bungeni jijini Dodoma, na kuongeza kwamba miaka ya nyuma wengi ambao walikuwa wanahamishwa kupisha maeneo ya uhifadhi walikuwa wengine wanatembea kwa miguu.

"Rais hili jambo amefanya la kibinadamu na utu sana na hakuna katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watu walioweza kuhama kwa raha kama wale wanaohamishwa kutoka Ngorongoro,"amesema Lusinde 

Tazama video hapa chini