Friday , 1st Jul , 2022

Baada kufanikiwa kuwanasa Romelu Lukaku na Kristjan Asllani kwa mkopo kutoka Chelsea na Empoli, klabu ya Inter Milan leo imekamilisha usajili wa mlinda mlango wa Cameroon Andre Onana toka klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi pamoja na kiungo Henrikh Mkhitaryan toka klabu ya AS Roma.

Andre Onana

Onana mwenye umri wa miaka26 amesaini mkataba wa miaka mitano na sasa anakua mrithi wa Samir Handanovic mwenye umri wa miaka 37, ambaye amedumu Inter Milan kwa muongo mmoja. Huku mchezaji wa kimataifa wa Armenia Mkhitaryan amesaini mkatawa miaka miwili kuitumikia miamba hiyo ya soka ya Italia.

Wachezaji hao wamewasili jijini Milan wakiwa wachezaji huru baada ya kandarasi zao na timu zao za awali kumalizika.

(Henrikh Mkhitaryan)

Wawili hao wameorodheshwa katika wachezaji waliuokamilisha uhamisho wao kwenye tovuti ya ligi kuu ya Italia ‘Serie A’  na kufanya mikataba hiyo kuwa rasmi hata kama Inter haijatangaza rasmi kuwasili kwao.

Pia Milan wameripotiwa kuwepo kwenye mazungumzo ya kumleta Paulo Dybala ambaye naye ni mchezaji huru akitokea Juventus baada ya kukataa kuongeza mkataba na klabu hiyo.