Tuesday , 5th Jul , 2022

Idara ya Uhamiaji nchini imeeleza kuibuka kwa watu maarufu kama vishoka ambao wamekuwa wakichukua fedha za wananchi kwa madai ya kwamba watawapatia passport kwa uharaka na kuonya idara hiyo haina uwakala mbadala na suala hilo linachafua taswira nzima ya mamlaka.

Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Paul Msele

Akizungumza na EATV Msemaji wa Idara hiyo Paul Msele, amesema vitendo hivyo havikubaliki na amewaonya wananchi wenye tabia hiyo kuacha mara moja.

Kuhusu watu wanaofoji viambatanisho vinavyomwezesha kupata passport, Msele amesema tatizo hilo limekuwa likisababisha usumbufu kutokana na baadhi ya wananchi kuleta viambatanisho bandia vinavyongiliana kimamlaka hasa kwenye vyeti vya kuzaliwa.