
Mfalme Zumaridi
Mawakili wa upande wa utetezi walitaka kuwasilisha hoja za mteja wao Zumaridi kutokuwa na imani na Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo lakini kutokana na Mahakama hiyo kuamua kupanga kesi hiyo kwa Hakimu mwingine wakaona hakuna haja ya kuwasilisha hoja hizo
Wakili upande wa serikali Emmanuel Luvinga, ameiambia Mahakama hiyo kuwa kutokana na upande wa utetezi kusema watawasilisha hoja hizo leo hawakuweza kuwaleta mashahidi mahakamani, hivyo kuomba kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu mkazi Clesensia Mushi ipangiwe tarehe nyingine
Akizungumza nje ya Mahakama wakili wa utetezi Linus Amri, ameshukuru uamuzi huo wa Mahakama wa kubadilisha Hakimu.