
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman ametoa kauli hiyo wakati akifunga kongamano la nne la kimataifa la nishati jijini Dar es salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kusema kuwa kwasasa mazingira ya uwekezaji ni shwari
Suleiman amewasihi wawekezaji kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta ya Nishati Kwa upande Zanzibar kwa kuwa mazingira ni rafiki na maeneo yapo yakutosha
Baadhi ya washiriki katika kongamano Hilo wamekiri kupata manufaa kutokana mijadala iliyofanyika huku baadhi ya kampuni zikipata tenda na mikataba mbalimbali ambayo yote inakwenda kusisimua uchumi wa nchi