Saturday , 13th Aug , 2022

Wananchi  Wilayani Ludewa Waliopisha Miradi Mikubwa  na Hazina ya Taifa ya Liganga na Mchuchuma  kwa  Miaka  Mingi Sasa wamesema wapo  tayari  kulipwa  fidia yao  huku  Serikali  ikisema  hatua za kulipa fidia hizo zimekamilika caada ya wananchi hao Kusubiri kwa mrefu

Taarifa za kulipwa fidia wananchi waliopisha mradi wa Liganga na Mchuchuma zilitolewa rasmi mapema mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kuwasili Mkoani Njombe ambapo Kituo hiki mara maada ya kuwasili wilayani Ludewa kwa  Wananchi waliopisha mradi

Akizungumza mwakilishi wa shirika la taifa la maendeleo NDC  Bw. Maundi amesema mapema mwezi huu serikali ipo tayari kuanza taratibu za kuanza kuwalipa wananchi walio pisha mradi huo huku Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Jamonga akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa uhakiki wa wananchi walio pisha maeneo ya mradi huo kwa muda mrefu