
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia leo Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Muhimbili, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.