Lori la mafuta lililoanguka Kongwa
Akizungumza na East Africa TV & Radio digital Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remedius Mwema Emmanuel, amesema kwamba mara baada ya kufika eneo la tukio walifanikiwa kuwatawanya wananchi waliofika eneo la tukio kwa ajili ya kuchota mafuta sambamba na kuwapa elimu juu ya athari zinazoweza kujitokeza.
"Tunaendelea kuondoa watu na kinachofuata ni kuliondosha hilo gari la mafuta hapa barabarani, tunashukuru wananchi tumefanikiwa kuwasogesza ili kuondosha maafa yanayoweza kujitokeza, watu wamekuja na ndoo lakini tumewafukuza na mimi nisingependa kuona wananchi wanachota mafuta," amesema DC Kongwa
Kwa mujibu wa DC Emmanuel amesema ajali ya lori hilo imetokea leo majira ya saa 1:00 asubuhi katika eneo la Majawanga wilayani humo wakati gari hilo likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Mwanza na lilipatwa na kadhia hiyo mara baada ya gari la Dangote kutaka kupita bila kuchukua tahadhari na ndipo ajali ilipotokea.