
Agizo hilo la mkuu wa mkoa kwa mkandarasi huyo limetokana na ujenzi huo ulioanza Juni mwaka huu ambao unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu kuonekana kusuasua, huku baadhi ya sababu zinazotajwa kuchelewesha kazi hiyo ikiwa ni pamoja na asili ya eneo la ujenzi kuwa na miamba mingi iliyosambaa, utetezi ambao mkuu wa mkoa hakubaliani nao
"Kabla ya mradi ilifanyika Survey, baada ya hapo kulikuwa na ushauri, ina maana mlishajua kwamba hapa majengo yanaweza kukaa, sasa mkishaanza halafu jengo likakataa ina maana taarifa za awali hazikuwa na msaada kwenye mradi, kwa hiyo sisi tunachukulia ulichosaini, moja ulikubaliana na fedha na pili ulikubaliana na mazingira haya na kila kitu" amesema Chalamila
Akitoa taarifa msimamizi wa mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni nne, Kafuku Maganga amesema kuwa una sehemu mbili za utekelezaji ambao unaanza na ujezi wa vyumba 12 vya madarasa, lakini akataja baadhi ya changamoto zinazochelewesha utekelezaji wa mradi huo
"Changamoto ya kwanza ni kukosekana kwa umeme mahala pa kazi, asili ya eneo ina miamba mingi iliyosambaa hali inayomtaka mkandarasi kuchoronga miamba kwa ajili ya ujenzi wa nguzo ili kuimarisha jengo na kutumia muda mwingi katika utekelezaji wa kazi, na misingi kuwa mirefu kutokana na eneo kuwa na mtelemko mkali" amesema Maganga