
Malalamiko hayo wametoa kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo wamesema pia kuna baadhi ya madereva wa magari ya abiria wanaendesha mwendo kasi hivyo wanaiomba serikali kushughulikia swala hilo ili kuzuia ajali zenye athari zaidi kwa binadamu
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Tanganyika, Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Onesmo Buswelu amewataka Madereva wa serikali na magari binafsi kuzingatia sheria za barabarani