Monday , 22nd Aug , 2022

Polisi watatu katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wamesimamishwa kazi kutokana na video iliyozaagaa mitandaoni ikiwaonesha wakimpiga mshukiwa mmoja huku wamemlaza chini 

Mmoja wa maofisa ameonekana akimpiga mtu huyo kichwani mara nyingi huku akimpigiza kichwa kwenye sakafu

Ofisa mwingine wa polisi ameonekana amepiga magoti  huku anampiga mshukiwa huyo  

Mtu huyo baada ya kupigwa alionekana akijikinga kichwa chake kwa mikono yake huku akijibiringisha barabarani kujilinda

 
Video hiyo imetazamwa na mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kuzua minongóno  

Mtu huyo aliyekamatwa alikua na tuhuma za kusababisha vitisho kwenye duka moja, ambapo  polisi walipigiwa simu kuja kumkamata alijihami kwa kumsukuma askari mmoja aliyeanguka chini