Wednesday , 24th Aug , 2022

Maelfu ya watu nchini Afrika Kusini wameandamana kupinga ongezeko la gharama za maisha 

Muungano wa vyama viwili vikubwa nchini humo unaongoza maandamano hayo  ambayo yananuia kupinga ukosefu mkubwa wa ajira, kupanda kwa bei ya mafuta na umeme. 

Maandamano hayo yanatarajiwa kuenea katika majimbo mbalimbali haswa ya   Cape Town na  Pretoria.
Maandamano hayo yanaitaka serikali kupunguza gharama za mafuta ikiwemo pia kupunguza kodi ya kwenye mishahara.  

Takribani theluthi ya watu nchini afrika kusini hawana ajira, huku nchi hiyo ikiingia kwenye mzozo wa kiuchumi uliosababishwa na vita ya Ukraine na Russia ikiwemo madhara ya UVIKO 19.
Serikali imesema kuwa inafanyia kazi madai hayo.

Waadamanaji wamesema kwamba wataendelea kuandamana mpaka pale watakapopata majibu ya uhakika