Thursday , 25th Aug , 2022

Magreth Magabilo, mkazi wa Area A Umonga Jijini Dodoma, anaomba msaada wa kupatiwa matibabu kutokana na kupata ajali ya barabarani miaka 20 iliyopita ambayo imemuacha na ulemavu wa mgongo, kushindwa kusimama, huku fuvu lake la kichwa likiwa limeingia ndani.

Magreth Magabilo

Magreth aliiambia EATV kuwa alianza kuhangaika kutafuta matibu katika hospitali mbalimbali na alipoona hali inakua ngumu ilibidi ajifanye na yeye ni muhanga wa ajali ya Treni ya mwaka 2002 Jijini Dodoma ili aunganishwe na majeruhi wa ajali hiyo lengo likiwa ni kupatiwa  matibabu jambo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kidogo.

Kwa sasa maisha ya Magreth ni ya kulala muda wote na kumaliza mahitaji yake yote ya kibinadamu kitandani na wanaye pekee wa kiume ndio msaada kwa kushirikiana na wasamalia wema wanaomsaidia kumuogesha, kumvalisha nguo na kumsitiri pindi anapohitaji huduma za kibinadamu.

Namba ya simu ya kumsaidia Magreth Magabilo ni 0759233513