
kikosi cha Singida Big Stars .
Big Stars imewasili jijini Mwanza leo Agosti 24, 2022 jioni ikitokea mkoani Singida na kupumzika wilayani Misungwi kabla ya kuanza programu za maandalizi ya michezo hiyo.
Timu hiyo itakipiga na Geita Gold Septemba 14 kisha kuivaa Kagera sugar Septemba 28 mechi zote zikichezwa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kabla ya hapo itawaalika Dodoma Jiji katika Uwanja was Liti mkoani Singida Septemba 11.
Akizungumzia kambi hiyo, Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Massanza amesema lengo ni kutengeneza mazingira ya wachezaji wake ambao wengi ni wageni kuzoea mazingira ya jiji la Mwanza itakapopigwa michezo hiyo.
Massanza amesema pia watatumia kambi hiyo kwa mapumziko ya muda mfupi kupisha mechi za timu ya taifa (Taifa Stars) kusaka nafasi ya kufuzu michuano ya CHAN huku wakitarajia kutambulisha wachezaji wapya wawili.
"Tumewasili salama jijini Mwanza tupo kwa mapumziko mafupi na kufanya maandalizi kwa ajili ya michezo ijayo na kutengeneza hali ya wachezaji wetu kuzoea mazingira na hali ya hewa ya huku ikizingatiwa kuwa tuna michezo miwili dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold yote ikichezwa hapa Mwanza,"