
Soba Sangánya, mdau wa vijana
Akizungumza na EATV Soba Sangánya ambaye ni mdau wa vijana ambapo amesema asilimia 60 ya watu kwa hapa Tanzania ni vijana, hivyo huwezi kuwatenganisha na kushika hatamu iwe katika uongozi ama kazi mbalimbali,
“Vijana ili waweze kuwa na maadili ya kazi ni vyema kuwajengea uwezo wa maarifa mbalimbali,yakiwemo ya utendaji wa kazi na uzalendo kwa taifa.
Ameongeza kuwa mabadiliko ya vijana kimaadili yanahusisha msukumo wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kijana anaenda katika mstari ulionyooka.
Kwa upande wake Kanani Mushi ambaye ni kijana akizungumza na EATV amesema vijana walio katika zama za utandawazi watumie fursa za mitandao katika masuala ya kujenga na kutafuta fursa mbalimbali ndio msingi wa kupata ajira.