Monday , 5th Sep , 2022

Mahakama Kuu nchini Kenya, hii leo Septemba 5, 2022, majira ya saa 6:00 mchana itatoa maamuzi katika kesi ya kupinga matokeo ya Rais iliyowasilishwa na aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais nchini humo Raila Odinga.

Raila Odinga na William Ruto

Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya Mahakama, na kwamba jumla ya Majaji saba wa Mahakama hiyo wanatarajiwa kutoa uamuzi wa kesi hiyo.

Majaji hao ni Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Isaac Lenaola, Smokin Wanjala, Ibrahim Mohammed, Njoki Ndungu na William Ouko.

Tume ya Uchaguzi ya IEBC nchini humo kupitia Mwenyekiti wake Wafula Chabukati, ilimtangaza William Ruto kuwa ndiyo mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura milioni 7.1, na kumshinda mpinzani wake Raila Odinga aliyepata kura zaidi ya milioni 6.