Monday , 5th Sep , 2022

Jeshi  la Polisi mkoani Mbeya, limetangaza operesheni ya kuwakamata madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakataokuvunja sheria za usalama barabarani ikiwemo kupita  kwenye taa za kuongoza magari bila kufuata utaratibu

Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Mkoa wa  Mbeya,  Abdi Issango  ametoa kauli hiyo kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi, Ulrich Matei  wakati akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva hao.
Mkuu Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya, Yussuph Kamota amewataka madereva  hao  kuheshimu sheria za usalama barabarani.

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva bodaboda Jiji la Mbeya, Aliko Fwanda alimehakikishia Jeshi la Polisi kwamba  watazingatia sheria zote za usalama barabarani