Tuesday , 6th Sep , 2022

Ukatili wa kiuchumi unaofanywa na baadhi ya wanaume wa Kata za Nzera na Kakubiro, Mkoa wa Geita wakati wa msimu wa mazao, unasababisha kufanyiwa ukatili wa kingono pindi msimu wa mazao unapomalizika

Wakizungumza leo Jumanne Septemba 6,2022 wakati wa mafunzo kwa kamati za Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (Mtakuwa) yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la kusaidia watoto yatima na wale walio kwenye mazingira magumu (SATF) baadhi ya wanaume wamedai kunyimwa unyumba na wenzi wao

Wanawake wamedai uamuzi wa kuwanyima wenzi wao tendo la ndoa unatokana na wanaume kuhama nyumbani msimu wa mazao na wanapomaliza fedha za mazao hurudi wakiwa hawana kitu na kuanza kuwasumbua wake zao

“Mimi kama mama hata hiyo hamu ya kukutana nae sina wakati wa kilimo tumehangaika wote lakini tukivuna mwenye mamlaka ni baba na mbaya zaidi anabeba mazao anaenda kuuza na kustarehe na wanawake wengine akimaliza hana kitu mfukoni ndio anarudi kwangu hiyo hamu napata wapi,” amesema Plukeria James