Wednesday , 14th Sep , 2022

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi, amelishauri Bunge kama ikiwezekana yafanyike majadiliano ambayo yatasaidia uanzishwaji wa viwanda vitakavyochakata mmea wa bangi na kupunguza makali ili uweze kutumika na kukuza pato la Taifa.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi

Kauli hiyo ameitoa hii leo wakati akitoa mchango wake katika muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 2 ya mwaka 2022 uliowasilishwa hii leo kwa mara ya pili na Mwanasheria Mkuu wa serikali Dkt. Feleshi.

"Kwanini suala hili la bangi tusilichukue tukajadiliana ili ikiwezekana tui-process na tujenge viwanda ambavyo vitapunguza makali ya bangi na itumike kwenye maeneo mbalimbali, wako watu wakitumia wanalima zaidi na mwingine anavuta tu kama sigara," amesema mbunge Jackline Msongozi