Friday , 16th Sep , 2022

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa maelekezo kwa wataalam wa dawa wakiwemo wafamasia kuzingatia miongozo ya utoaji wa dawa na kuhakikisha mwandiko unasomeka kwakuwa kutokufanya hivyo kunahatarisha afya za wagonjwa.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume anasisitiza na kuwaagiza wataalam kuzingatia muongozo wa utoaji dawa ili kutowadhuru wagonjwa na jamii ikiwa ni siku moja kabla maadhimisho ya siku ya usalama wa wagonjwa duniani yanayofanyika kila Septemba 17.

“Siku hii ya usalama wa mgonjwa ni mhimu kwasababu inakumbusha umma na jamii yote kuzingatia miongozo katika utoaji na utumiaji wa dawa, hii ni mhimu kwasababu kutokufanya hivuo kunapelekea matumizi ya dawa yasiyosahihi ambayo hugeuza dawa kuwa sumu na kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa ikiwa ni oamoja na ulemavu wa viungo kama Ini na Figo”- Dkt. Rashid Mfaume, Mganga Mku Mkoa wa Dar es Salaam.

 Aidha, katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Wafamasia Tanzania kwakushirikiana na washikadau wa afya, Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania Bw. Fadhili Hezekiah ametoa ufafanuzi wa kitaalam kuhusu dozi ya 1 × 3 ambayo anadai haishauriwi kitaalam.

“Kimsingi uandishi wa dawa 1 × 3 haupaswi kisheria, kikanuni na kitaaluma. Unaposema 1 × 3 maana yake dawa itumiwe Mara tatu ndani ya saa 24, hii inamanisha kila baada ya saa 8 dawa ile iweze kutumika. Na hii nisehemu ambayo tunatakiwa kuifanyia marekebisho na kuiangalia kama wafamasia ikiwa ni pamoja na kusisitiza katika uandishi mzuri wa vyeti vya dawa na hii inapelekea kwamba 90% ya vyeti vinaandikwa kimakosa"- Fadhili Hezekiah, Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania.