Friday , 16th Sep , 2022

Waziri wa habari Nape Nnauye ameitaka Mamlaka ya mawasiliano kuona namna ya kuandaa tuzo maalum Kwa watu watakaoweza kuzalisha maudhui bora ya ndani na kuipa thamani pamoja na kuweka utaratibu na kanuni zitakazowatambua wazalishaji binafsi Ili watakaofanya vizuri maudhui yao yatumike.

Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari

Waziri Nape ametoa rai hiyo  wakati akifungua mkutano uliokusanya kamati ya maudhui ya ndani kutoka TCRA, vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu ya habari, waandishi, wazalishaji wa filamu sambamba na wimiliki wa mitandao wanazalisha na kusambaza Habari.

Nape amesema tuna Lugha ya pekee ya kiswahili ambayo kama wadau wataamua kuitumia inaweza kupata maudhui ambayo yatauzwa nchi katika nchi zote za SADC huku Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA akisema lengo ni kufikia uchumi wa kidigitali ili kuendelea kukuza maudhui ya ndani.