Mchezaji wakulipwa kutoka Lugalo Frank Mwinuka wa Lugalo ameibuka na ushindi kwa mikwaju 140 akifuatiwa na Elsante Lembres kwa Mikwaju 144,huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Nuru Mollel wote kutoka Arusha Gymkhana kwa Mikwaju 146.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mchezo Mwinuka amesema siku ya Kwanza alipata Mikwaju 72 na Siku ya Pili mikwaju 68 na anatarajia kufanya vizuri Zaidi Mashindano yajayo huku kwa wachezaji wa wa Ridhaa Ally Mcharo wa TPC ameongoza kwa siku ya Kwanza ya Mchezo kwa Mikwaju 71.
Kwa upande wake Nahodha wa klabu ya TPC Moshi Mkoani Kilimanjaro ambao ndio wenyeji wa mashindano hayo Jafari Ally amesema, Shindano linaendelea vizuri na muitikio wa wachezaji ni wakuridhisha.
Shindano la TPC Open 2022 limeanza kutimua vumbi siku ya jana kwa wachezaji wa Kulipwa na Leo kwa Wachezaji wa ridhaa ,ambapo Wachezaji Zaidi ya 90 kutoka vilabu mbalimbali wameshiriki shindano hilo.

