Monday , 19th Sep , 2022

Polisi mkoa wa Iringa, wanamshikilia Michael Mbata, mkurugenzi wa kampuni ya Foa Motors kwa tuhuma za makosa ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha milioni 150, kutoka kwa wakazi wawili mkoani humo kwa ahadi ya kuwaagizia magari aina ya Howo kutoka Japan na kisha kuzima simu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi, akionesha magari aliyokutwa nayo mtuhumiwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi, amesema kuwa mara baada ya mtuhumiwa kukamatwa alikutwa na magari mawili aina ya Nissan Dualis na Subaru Impreza ambayo ni tofauti kabisa na yale aliyoagizwa na wateja wake.
 
Katika hatua nyingine pia jeshi hilo linamshikilia Alex Peter, kwa kukutwa na vipande 10 vya meno ya Tembo vikiwa kwenye mfuko wa salfeti maeneo ya mlimani Kinyanambo A wilayani Mufindi.