Thursday , 29th Sep , 2022

Shirika la afya duniani limesema kwamba mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea nchini Uganda  haukugundulika mapema.

Uchunguzi umeonyesha kwamba mgonjwa wa mwanzo alipaswa kugundulika mapema kwa dalili alizokua ameonyesha tangu mwezi  August 2022 , lakini hakutiliwa maanani kama mgonjwa wa Ebola. 

Takribani watu 24 wamekutwa na maambukizi ya ugonjwa huo  huku wengine wanne wakipoteza maisha. 

Dkt Patrick Otim, ambaye anachunguza Ebola nchini Uganda  amesema kwamba kutakua na ugumu wa kutokomeza kabisa ugonjwa huo, sababu wakati unaripotiwa tayari watu wengi walikua wamehudhuria maziko ya watu waliokufa nao. 

Ameongeza kwamba ugonjwa huo umekua na dalili kama za  malaria na  typhoid.