
Bw.Harry Knoesen ( 64) alikua ni kiongozi wa kikundi cha kigaidi ambaye alipanga kuipindua serikali mnamo tarehe 28 Novemba 2019 , akitumia silaha nzito kama AK-47 , mabomu ya kurushwa kwa mkono na silaha nyinginezo.
Mahakama kuu ya Mpumalanga nchini humo imeelezwa kwamba Knoesen pia alipanga kutumia silaha za kibaiolojia ili kuwaua watu weusi .
Kwa mujibu msemaji wa wa mamlaka ya mwendesha mashata wa taifa Bi.Monica Nyuswa,ilidaiwa kwamba alitaka kufanya mambo hayo kwa kuwa aliagizwa na Mungu kuirejesha Afrika Kusini kwenye mikono ya watu weupe.