
Rais Samia Suluhu Hassan
Taarifa ya uteuzi huo ilitolewa usiku wa kuamkia leo Oktoba 3, 2022, ambapo pia amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula.
Aidha amemteua Angellah Jasmine Kairuki, kuwa Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).