Monday , 3rd Oct , 2022

Serikali imewataka wafugaji wa asili nchini kuanza kulima malisho ya mifugo yao,ambayo yaliathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na kupelekea idadi kubwa ya mifugo kufa kutokana na kukosa malisho ili waweze waondokana na athari hizo kwa siku zijazo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anaeshulikia sekta ya mifugo Tixon Nzunda

Hayo yamesemwa na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anaeshulikia sekta ya mifugo Tixon Nzunda wakati akizungumza na wafugaji wa asili waliyopanga katika ranch ya taifa ya west kilimanjaro na kuwataka wafugaji hao kulima malisho.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ranchi za taifa   Peter Msofe amesema bodi ya ranchi za taifa wameamua kufanya mabadiliko ya ufugaji  ili kuhakikisha wanakuwa na vituo vya umahiri katika uzalishaji.

Nao baadhi ya wafugaji wa asili waliyopanga katika ranchi hiyo wameiomba serikali kuwaongezea muda wa kupangisha huku wakiiomba serikali kukiangalia kiwanda kilichopo namanga.