Friday , 7th Oct , 2022

Serikali kupitia Wizara ya Habari imesema itahakikisha wabunifu kwenye sekta ya TEHAMA, wanachangia uchumi wa nchi yao kwa kuongeza ajira kwa vijana kwani sekta ya mawasiliano nchini ina fursa kubwa kuweza kuongoza kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati kwenye soko la ajira.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi, ametoa kauli hiyo leo Oktoba 7, 2022, jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliowashirikisha, wabunifu kwenye sekta ya TEHAMA uliolenga kuona namna bora ya kuzisaidia kampuni hizo za ubunifu kuweza kufanya biashara.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za kidigitali kutoka kampuni ya simu za mkononi nchini ya Vodacom Nguvu Kama do amesema Vodacom imeanzisha programu maalum inayofahamika kama Vodacom digital accelerator ambayo imelenga kuwasaidia vijana walioonyesha dhamira ya ubunifu kwenye uchumi wa kidigitali 

Kwa upande wake mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu huria Cha Dar es Salaam Dkt. Cosmas Mnyanyi, ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya elimu maalum, ameshauri sekta ya TEHAMA isiwaache nyuma watu wenye mahitaji maalum.