Sunday , 9th Oct , 2022

Mtoto  mwenye umri wa miaka mitatu aitwae Emmy ,alikua amesinzia huku amemuegemea rafiki yake darasani  katika shule iliyoshambuliwa kwa risasi huko Kaskazini mwa Thailand , wakati muuaji alipovunja mlango na kuingia ndani alhamis wiki hii.

 

Darasa hilo lililokua na wanafunzi takribani 11 wote wenye umri wa miaka mitatu , walikua wakiendelea na kujifunza kuchora na  kuandika , ambapo ilipofika saa 4 asubuhi saa za nchi hiyo, mwalimu wa darasa alituma picha za watoto hao kwa wazazi wao ili kuonyesha kwamba wapo kwenye siha njema.

Saa mbili baadae mtu mwenye silaha aliyetambulika kwa jina la  Panya Kamrab , aliingia kwenye darasa hilo na kufyatua risasi ya kwanza iliyomuua mwalimu wa darasa aliyekua na ujauzito w amiezi 8, kisha muuaji huyo  alianza kufyatua risasi kwa wanafunzi hao na kuwaua marafiki wa Emmy wakati yeye amesinzia.

 Bila kujua kilichojiri, Emmy aliamka na kuhisi wenzake wamelala, ambapo polisi walimuwahi na kuifunika sura yake ili asione damu zilizokua zimepatakaa darasani.

Emmy ni mtoto pekee aliyepona mauaji hayo mabaya nchini humo , tukio lililojiri Alhamisi wiki hii na kuua watu 37.