
Hayo yameelezwa leo Oct 10, 2022 na Rais Samia Suluhu Hassan akitoa taarifa ya waliyojadili na Rais wa Kenya Wiliam Ruto Ikulu jijini Dar es salaam.
“Tulikubaliana kuwataka wataalam wetu kufanyia kazi vikwazo vya kibiashara vilivyopo baina ya Kenya na Tanzania na kwa ujumla wataalam walitambua vikwazo 68, ambavyo vilifanyiwa kazi vikwazo 54 viliondoka visivyo vya kikodi na bado kuna vikwazo 14 vimebaki na tumetaka mawaziri wetu wa sekta ya biashara na uwekezaji wakutane kwa haraka kufanyia kazi vikwazo 14 ili tuwe na uhuru mpana wakufanya biashara”.
Kwa upande wake Rais Ruto amesema katika kuenzi misingi iliyojengwa na waliyowatangulia, Rais Nyerere na Rais Jomo Kenyata wataunganisha watu wa Jumuiya yaAfrika Mashariki kwa pamoja kuweza kufaidika nchi hizo mbili”
Rais Ruto yupo hapa nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya siku mbili akiambatana na mke wake Rachel Ruto.