
Meneja wa TANESCO Kanda ya Magharibi Mhandisi Richard Swai wakati akizungumza na watumishi wa shirika hilo katika Mkoa wa Tabora amesema miongoni mwa malengo muhimu ya shirika hilo ni pamoja na kufikisha huduma maridhawa kwa wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora Mhandisi Hadija Mbaruku amesema pamoja na mipango mingi katika uwajibikaji waliyonayo wamejipanga kuhakikisha wananchi wanafikishiwa huduma kwa wakati bila vikwazo .