Monday , 10th Oct , 2022

Wanyamapori na viumbe hai walipo katka hifadhi ya Taifa ya Ruaha vipo hatarini kupoteza maisha baada ya Mto wa The Great Ruaha kukauka ambao kimsingi ndio roho ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Picha ya mto Ruaha Mkuu

Miongoni mwa sababu za kukauka mto huo zikitajwa kuwa ni pamoja na kukithiri kwa shughuli za kibinadamu katika bonde la Usangu hususani eneo la Ihefu Wilayani Mbarali mkoani mbeya.

Akizungumza na kituo hiki Muikolojia wa hifadhi ya Taifa Ruaha Norbet Wanzara amesema kutokana na maji kukauka katika mto huo tayari wanyamapori wanao tegemea maji ya mto huo moja kwa moja wameanza kuhaha huku wanyamapori wakubwa wakilazimika kutoka nje ya eneo la hifadhi kutafuta maji.

September 30 mwaka huu katika eneo la Ikoga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera alitangaza kuanza kwa operesheni ya kuondoa mifugo yote katika bonde la Ihefu na pengine hali ya mto huo ndio sababu ya operesheni hiyo.

Hata hivyo kukithiri kwa uvamizi katika bonde la Ihefu kumetajwa kuchangia uharibifu mkubwa wa ikolojia ya eneo la hifadhi ya Ruaha.