
Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha masuala ya usalama mtandaoni kutoka Wizara ya Mawasiliano Steven Wangwe
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji elimu ya masuala ya usalama mtandaoni katika shule ya sekondari Jangwani Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha masuala ya usalama mtandaoni kutoka Wizara ya Mawasiliano Steven Wangwe amesema bado watanzania wengi hasa vijana wanakabiliwa na changamoto ya matumizi yasiyofaa ya mitandao na kuahidi kuendelea kutoa elimu kwao.
Kwa upande wake mwakilishi wa shule ya Sekondari Jangwani Mwalimu Philip Kilipamwambu amesema kwa sasa hakuna somo la elimu ya masuala ya usalama mitandaoni licha ya wanafunzi wengi kuendelea kujifunza matumizi ya vifaa vya TEHAMA.
Nao wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wanabainisha kuwa bado wanafunzi wengi wanakosa elimu ya masuala ya usalama mtandaoni licha ya idadi kubwa ya vijana kujihusisha kazi mitandao kitu ambacho kina hatarisha maadili ya vijana wengi.
Hayo yanajiri katika maadhimisho ya mwezi wa elimu ya masuala ya usalama mitandaoni.