Monday , 17th Oct , 2022

Vifurushi vya mabegi  ya plastiki ya dawa vilivyosombwa na maji ya bahari vimekutwa ufukweni huko Wales .

Taarifa za polisi wa nchi hiyo zinasema kwamba Virufushi hivyo vyenye thamani ya mabilioni ya fedha vimekutwa kwa idadi kubwa ya mifuko myeusi iliyofungwa kwenye  plastiki ambavyo viligundulika na wapita njia kwenye ufukwe wa Tan-y-Bwlch karibu Ceredigion, tarehe 1 Oktoba.

Vifurushi  zaidi vilipatikana baadaye na vyote vinadhaniwa kuwa na dawa za kulevya aina ya  cocaine. Polisi wa Dyfed-Powys  wamewaonya wananchi kutogusa tena kifurushi chochote iwapo kitasombwa na maji kuelekea ufukweni , bali kuwasiliana na jeshi hilo.

 Inasemekana zaidi ya kilo 1,200 za cocain zimekutwa kwenye vifurushi hivyo.