Friday , 21st Oct , 2022

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema serikali itapanga vikosi kadhaavya watunga sheria kuangalia siasa na katiba na huenda wengine wakatoka katika kikosi kazi alichokiunda kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ameyasema hayo mara baada ya kupokea mapendekezo ya ripoti kikosi kazi cha kuratibu na kuchakata maoni ya wadau wa demokrasia kutoka kwa mwenyekiti Profesa Rwekaza Mukandala. akibainisha kuwa mapendekezo yao sio amri kwa serikali ingawa ameahidi kuyafanyia kazi

Amesema yapo mambo ambayo serikali inaweza kuyafanyia kazim kwa haraka na mengine kutazama kama sheria zilizopo kama zina upungufu wa kuyashughulikia

Hata hivyo, Rais Samia amesema sio jambo la kukabidhiwa papo uanze kulifanyia kazi, lakini kikosi kazi kimependekeza mambo mazuri yanayotakiwa kuzingatiwa na kuyafanyia kazi katika utendaji wa Serikali huku Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini, kimependekeza vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vipatiwe asilimia 10 ya ruzuku inayotengwa kila mwaka wa fedha.

Awali akiwasilisha mapendekezo hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala Amefafanua ili chama kipate ruzuku hiyo, lazima kiwe na usajili kamili, kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuthibitisha kinakidhi matakwa na chama kiwe kimeshiriki uchaguzi mkuu angalau mara mbili tangu kimepata usajili kamili.

Vilevile, amesema chama kisiwe kimepata hati chafu baada ya kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka uliopita na ruzuku itumike kwa shughuli za kuendesha ofisi ya makao makuu, ofisi ndogo.