Wednesday , 26th Oct , 2022

Mamlaka katika jimbo la Imo nchini Nigeria zimetakiwa kumkamata mwanamume anayedaiwa kumshambulia na kuvunja mkono wa mtoto wake wa miezi miwili.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 31 anaripotiwa kumshambulia mtoto wake kwa kutumia kitambaa cha plastiki  sababu zinazotajwa kuwa ni kichanga hicho kuleta usumbufu wakati mwanaume huyo amelala .

Mke wa mwanaume huyo ameviambia vyombo vya habari kwamba mumewe  alichukua simu yake na kumfungia yeye na mtoto katika chumba kimoja na kumtishia kutowaambia majirani. Hatimaye alitoroka siku mbili baadaye na kumpeleka mtoto wake hospitalini ambako madaktari walimkata mkono.

Dkt Chiedozie Mbalewe ambaye alimtibu mtoto huyo ameviambia vyombo vya habari kwamba kukatwa viungo hivyo kulifanyika ili kuokoa maisha ya mtoto huyo. Mtuhumiwa amekimbia na mama huyo ameripoti kesi hiyo polisi. Kundi la waandishi wa habari wanawake na tume ya kitaifa ya haki za binadamu wametaka haki itendeke.