Wednesday , 26th Oct , 2022

Janeth Charles (18), mkazi wa Mtaa wa Nyakahangola ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyabubele iliyopo Kata ya Kasamwa mkoani Geita amefariki dunia baada ya kunywa sumu ya panya kwa madai ya kwamba alikuwa mjamzito.

Jeneza lililobeba mwili wa mwanafunzi huyo

Baba wa marehemu  Charles Lugwesa, amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:00 jioni baada ya binti huyo kudai anasumbuliwa na tumbo hali ambayo iliwapelekea wazazi wote wawili kumchukua na kumpeleka zahanati ambako alipewa matibabu kwa muda mfupi na kufariki.

Taarifa zimeeleza kwamba, awali kabla mauti hayajamfika, mwanafunzi huyo alimwambia daktari kwamba amekunywa sumu ya panya na alipoulizwa sababu za kufanya hivyo hakujibu chochote.

Kwa upande wake viongozi wa dini na serikali ya kijiji cha Nyakahongola, wamewataka wazazi kutokuwa wakali kwa watoto wao wanapopata changamoto ili kuepusha kujichukulia maamuzi magumu.