Wednesday , 26th Oct , 2022

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella, amewataka wataalam wanaosimamia miradi ya maji kuacha kukaa ofisini na badala yake kwenda katika maeneo wanayotekeleza miradi  hiyo na kufanya tafiti za kutosha ili kuepuka kufanya kazi zisizokuwa na ubora pamoja na ufujaji wa fedha za serikali

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella

RC Mongella ametoa agizo hilo wakati alipotembea moja ya mradi wa maji katika Kijiji cha Mfulonyi wilayani Arumeru unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), ambapo amebainisha kuwa mradi huo una mapungufu hivyo hautakuwa na  tija kwa wananchi.

Nae Meneja wa RUWASA katika wilaya ya Arumeru Mhandisi Shabiri Waziri, ameeleza changamoto inayosababisha mradi huo kuchelewa kukamilika huku baadhi ya wakazi wakiomba kupewa kipaumbele katika suala la maji.