
Bunge la Gambia
Katika uchunguzi wa awali, watoto walipatikana na matatizo makubwa ya figo. Kikao cha leo Jumatano katika bunge kitakuwa ni cha kwanza cha wabunge nchini humo tangu mkasa huo ulipotokea mapema mwezi huu.
Maafisa nchini Gambia wamesema hakuna visa vipya zaidi, lakini kuna visa 82 vilivyopo na 12 walipona wakati vingi kati ya visa vilivyopo vinahusisha watoto wenye umri wa mwaka mmoja na miaka miwili ambao walitumia dawa hizo za kikohozi zilizozalishwa na kampuni moja ya nchini India.
Mashirika ya kiraia nchini humo yanaongeza shinikizo kwa mamlaka ya serikali kuchukua hatua dhidi ya wale waliohusika na uagizaji wa madawa hayo yaliyoibua taharuki katika jamii ya taifa la Gambia wakati maafisa wa afya na shirika la Msalaba Mwekundu wameanza awamu ya pili ya kuitisha dawa hizo za kikohozi ili zisitumike.
Wakati huohuo uchunguzi wa polisi tayari umebaini kuwa Shirika la udhibiti wa madawa lilianzishwa kufanya kipimo cha usalama wa madawa huku Rais Adama Barrow akiweka tume ya uchunguzi kuchunguza vifo hivyo.