
Waziri wa Nishati January Makamba
Waziri Makamba ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu mradi wa gesi asilia wa LNG ambao Tanzania ilishasaini makubaliano yake ya awali.
Aidha Waziri Makamba ameeleza faida za utekelezwaji wa mradi huo kwa taifa letu, ikiwa pamoja na kupatikana kwa ajira zaidi ya laki nne.
Kwa upande wa wadau kutoka sekta binafsi wameishukuru serikali kwa kuelendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji huku wakieleza uwekezaji mkubwa kwenye Mradi wa LNG ni funzo wa wawekezaji wazawa.