Thursday , 27th Oct , 2022

Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (Ant drug Unit), limekamata jumla ya watuhumiwa 1212 wa madawa ya kulevya pamoja na kukamata tani 1.96 za bangi, tani 1.08 za mirungi, pamoja na heroini gramu 448.74.

Bangi

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Jeshi hilo kuendesha opersheni nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu hadi Oktoba 25 ambapo pia katika operesheni hiyo mashamba ya bangi hekari 9.55 na miche ya mirungi ipatayo 220 iliteketezwa.

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 27, 2022, na Mkuu wa Kitengo cha kuzuia dawa za kulevya nchini Makao Makuu ya Upelelezi, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Amon Kakwale.