
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema jambazi huyo alikamatwa na pisto aina ya Broin yenye namba A 920 580 ikiwa na risasi 9
Kamanda Maigwa amesema uchunguzi wa awali umebaini silaha hiyo inamilikiwa na mtu ambae jina limehifadhiwa na iliibiwa kwa mmiliki huyo ambae ni mkazi wa Manyara
Jambazi huyo alikamatwa pia na silaha aina ya Sime ambapo mtuhumiwa alifariki wakati akipelekwa Hospitalini na mwili wake umehifadhiwa katika hiospital ya kanda ya KCMC Moshi