Friday , 28th Oct , 2022

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillius Wambura, leo Agosti 28, 2022, amemuapisha SACP Suzan Kaganda, kuwa Kamishna wa Polisi na Kamishna wa Kamisheni ya Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, nafasi ambayo ameteuliwa na Rais Samia hivi karibuni.

CP Suzan Kaganda, wakati akila kiapo

Mara baada ya kumuapisha, IGP Wambura amemuelekeza CP Kaganda kusimamia kwa dhati maslahi ya jeshi na askari wote kwa ujumla, kukemea vitendo vya rushwa, kusimamia weledi kwa kuhakikisha kuwa maafisa, wakaguzi, askari na watumishi wanapata mafunzo ya kujiendeleza mara kwa mara.

Aidha CP Kaganda pia ameelekezwa kusimamia utekelezwaji wa kauli mbiu ya jeshi hilo kwa vitendo pia na kuwa chachu na kuwasimamia maofisa wakaguzi na askari wa kike ili na wao waweze kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa kujiamini kama wafanyavyo wanaume.

CP kaganda anakuwa ni Kamishna wa pili wa kike kushika nafasi ya Ukamishna kwa jeshi la polisi tangu uhuru hadi sasa, akitanguliwa na Kamishna mstaafu Elice Mapunda, aliyekuwa Kamishana wa Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi 2015 hadi 2017 alipostaafu.