Friday , 28th Oct , 2022

Mlipuko wa moto umeteketeza hekta za vichaka katika mlima Longonot nchini Kenya, ambao ni maarufu kwa wapanda milima katika eneo la Bonde la Ufa.

Shirika la Wanyamapori la Kenya (KWS) linasema katika taarifa kwamba lilizima moto huo ulianza kuwaka siku ya Alhamisi.

KWS ilikanusha uvumi unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kumekuwa na mlipuko wa volkano, na kusema inataka "kuhakikisha kuwa bustani hiyo ni salama kwa wageni wote".

Mlima huo ambao ni volkano ya dormant, umekuwa moja ya mada zinazozungumziwa sana katika mtandao wa Twitter, huku baadhi ya watumiaji wakidai kuwa walikumbwa na mitetemeko ya ardhi kutokana na mlipuko unaodhaniwa.

Chanzo cha moto huo mlimani bado hakijabainika.Mwaka jana, mlipuko kama huo wa moto ulipunguza sehemu ya mimea katika hifadhi hiyo hadi majivu.