
Kamanda Jongo ameyasema hayo wakati wanamuaga aliyekuwa mkuu wa Dawati la Jinsia kituo cha Polisi wilaya ya Geita Hidaya Mrisho na kuwahasa maaskari wa kike kuwa Dawati bila askari wa kike haliwezi kufanikiwa.
"Polisi wanawake ni chachu katika Dawati la Jinsia na watoto na nyie wote mtakuwa ni mashahidi, kwamba jinsi Dawati linavyofanya kazi bila Police Tanzania Female Network hatufiki, kweli si kweli, na naomba nichukue nafasi hii kuwasihi, askari wenzangu wa kike wa mkoa wa Geita, tusiliacje Dawati ni la kwetu kwa sababu wewe ukiwa mama huwezi kukubaliana na ukatili kwahiyo utafight kama mama, utafight kama Askari, lakini utafight kama mwamakitengo cha Dawati la jinsia na watoto", alisema Jongo.
Kwa upande wake aliekuwa mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto D/DSST mstaafu Hidaya Mrisho amewaasa askari wa kike kuwa na ushirikiano ili waweze kufanikisha jamii isiyokuwa na vitendo vya Ukatili.
"Askari wote, ambao bado mpo kazini mwenyezi Mungu awalinde, awaongoze, awajalie Hekima, Busara, awajalie utendaji mtende kama wenye imani mtafaulu kwa kila kitu", alisema Mrisho.
Baadhi ya wadau wa kupinga ukatili wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi ili kutokomeza vitendo vya kikatili mkoani humo.
"Sisi kama Plan International tutaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha tunajenga jamii salama isiyo na ukatili wa kijinsia lakini tunatambua kwamba uwepo wako hapa utasababisha kuwa na mazingira yenye kutambua haki na usawa kwa wasichana na wanawake wote", alisema Mashauri.