
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi
Prof. Makubi ameyasema hayo leo wakati alipokitembelea chuo hicho kufuatia malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa Wizarani.
Mara baada ya kuongea na watumishi hao Katibu Mkuu huyo akiwataka Viongozi wa chuo pamoja na watumishi wote kujitathimini na kuhakikisha chuo hicho kinaboresha ufundishaji kwa vitendo pamoja na uwajibikaji wa Menejiment hiyo kwa kuwa karibu na watumishi na wanafunzi
Hata hivyo Prof. Makubi alisema amekiweka chini ya uangalizi wa karibu kwa miezi mitatu chuo hicho ambacho ili kuweza kubadilika na kuwajibika ipasavyo ili kuzalisha wanafunzi bora katika kuhudumia afya za Wananchi. Uongozi umetakiwa unatakiwa kuwashirikisha watumishi katika maamuzi yao, madai na kuwasikiliza kwa karibu sana.