
Kampuni ya mchezo wa kubashiri Tanzania Parimatch imemtambulisha mwanamuziki wa kizazi kipya, Omary Ally Mwanga maarufu Marioo kuwa balozi wa kampuni hiyo leo Novemba 3, 2022 lengo likiwa kuwathamini wateja wao kwa kuwapa burudani zaidi.
Ujio huo wa Marioo kwenye kampuni namba moja ya kubashiri Tanzania Parimatch umekuja na ofa za kijanja na tovuti yenye muonekano mzuri na kasi kubwa huku ikiwa na uwezo mdogo wa intaneti na kwa wateja wao wataweza kushea mikeka yao kwa marafiki ili nao waweze kupata burudani kutoka Parimatch.
Akizungumza kwenye hafla ya utambulisho huo Mkurugenzi wa Parimatch, Erick Gerald amesema kupitia Balozi huyo wana uhakika ataipeperusha vyema chapa hiyo kila eneo pamoja na kusaidia kutoa uelewa kwa wachezaji wanaobeti ili wote waweze kufurahi na kucheza kistaarabu.
“Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Marioo kama balozi wetu kwa ajili ya kuzidi kupata burudani, yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza, Ila kikubwa ni kwamba huwezi ongelea burudani Tanzania bila ya kuacha kumtaja Marioo”, amesema Mkurugenzi wa Parimatch Tanzania, Erick Gerald.
Pamoja na hayo Mkurugenzi wa Parimatch amesema kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia Parimatch imewaandalia ofa kabambe wateja wake pamoja na wadau wote wa michezo ya kubashiri ambapo kwa kushiriki katika promosheni hizo, kutamfanya mchezaji ajishindie zawadi nono ambazo zitamfanya ajihisi kama yupo Qatar.
Pia Parimatch imewakumbusha watanzania pamoja na wadau wote wa kubeti kuwa Kampuni ya Parimatch ndiyo kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual.
Mbali na soka, kampuni hiyo pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match. Na zaidi ya yote kuna ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi!