
Hakimu Erasto Phili amesema kesi hiyo imedumu kwa muda mrefu na kuwataka upande wa Jamhuri kama cetifiketi zipo ni vyema zikawasilishwa mahakamani kwani hakimu mwenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo ambaye ni hakimu Salome Mshasha yupo mafunzoni kwa takribani wiki moja ili baada ya mafunzo hayo kesi hiyo ipate kusikilizwa
Hakimu phil ameihairisha kesi hiyo mpaka tarehe 21 mwezi wa 11 2022 na mshtakiwa ataendelea kuwa mahabusu