
Baadhi ya wakazi wa eneo ambalo limezingirwa na maji machafu ya mgodini
Ni wakazi wa vijiji vya Mwangolo na Nyenze, Kata ya Mwaduiluhumbo ambao wameiomba serikali kuwapa msaada wa haraka kutokana na nyumba zao kuzungukwa na tope lililotokana na bwawa la kuhifadhi maji machafu katika mgodi wa Williamson kupasuka na kutiririka kwenda kwenye makazi ya watu na kwenye mashamba
Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini nyumba 13 zimezungukwa na maji machafu pamoja na tope na tayari ameunda tume ili kujua kama kuna athari zaidi na chanzo cha bwawa hilo kupasuka.